Kozi hii inalenga kujenga stadi za ujasiriamali ambazo zitakusaidia kujikwamua kiuchumi katika nyakati hizi ambazo ajira ni adimu.
JoinDunia inaenda kasi sana na upatikanaji wa ajira unazidi kuwa mgumu hasa kwa vijana wanaohitimu vyuo vikuu na vya kati. Stadi za ujasiriamali zinaweza kuleta suluhu kwa tatizo la ajira katika nyakati hizi. Vijana wengi wameweza kujiajiri katika sekta mbalimbali kupitia ujasiriamali mdogo na wa kati na hivyo kutohitaji kuajiriwa bali wao wamekuwa sehemu ya kutatua tatizo la ajira kwa kuajiri vijana wenzao.
Lengo kuu la kozi hii ni "Kujenga uwezo wa kubuni miradi ya kuzalisha kipato"
Katika kozi hii utaweza kupitia vipengele vifuatavyo;
1. Maana na kanuni za ujasiriamali
2. Jinsi ya kupata wazo la biashara
3. Namna ya kufanya utafiti wa soko
4. Jinsi ya kuweka mpango wa mradi